Saturday 2nd, November 2024
@KATA ZA WILAYA YA ITILIMA
KATA YA MHUNZE
Wananchi wa Kijiji Cha Ngando, kilichopo katika kata ya Mhunze, Wilayani Itilima wakionyesha hali ya kuhamasika kushiriki kwa kujitolea katika ujenzi wa shule shikizi ya Msingi Ngando.
|
Mafundi na wasaidizi wao wakiwa katika ujenzi wa Jengo la Shule Shikizi ya Msingi Ngando, iliyopo katika kata ya Mhunze, wilayani Itilima. |
Kamati ya Elimu, Afya na Maji Ikiongozwa na Mwenyekiti Mhe. Robert F. Jongela ambaye ni Diwani wa luguru, imeridhika na kasi na Ufanisi wa Utekerezaji wa Miradi Mbali mbali inayo endelea Wilayani Itilima.
Kamati hiyo ikiwa katika kijiji cha Ngando, kilichopo katika Kata ya Mhunze, Ilishuhudia Mradi Uliyo fadhiliwa na EQUIP kwa Kiasi cha Shilingi Milioni 60/- ukihusisha wa Ujenzi wa Madarasa mawili, ofisi moja, matundu manne ya vyoo vya Wanafunzi na Matundu Mawili ya vyoo vya Watumishi, katika Shule hiyo Shikizi ya Msingi Ngando.
Afisa mtendaji wa Kijiji cha Ngando Bw. Amos Mkama akitoa maelezo mbele ya kamati ya Elimu, Afya na Maji ilipofika kuangalia maendeleo ya ujenzi wa Shule shikizi ya Msingi Ngando
|
Akitoa Ufafanuzi kuhusiana na Mradi huo Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Ngando Ndg. Amosi Mkama alisema Kabla ya ujenzi huu kulikuwa na Ujenzi wa Madarasa matato kwa Nguvu za Wananchi na Ufadhili Kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Itilima Mhe Njalu Silanga ambaye alitoa Mifuko ya Saluji 150 kufanikisha ujenzi huo wa awali.
Akitoa maelekezo, Mhe. Jongela alimtaka Mtendaji wa kijiji hicho kuhakikisha usimamizi unaendelea kuboreshwa ikiwezekana ujenzi huo ambao ulianza tarehe 1/7/2018 wa majengo hayo ukamilike kwa wakati muafaka, kama ulivyo pangwa na Wafadhili.
Kijiji cha Ngando kinaidadi ya wanafunzi wa darasa la 1-7 wasiopungua 1,200 ambao wanasoma katika shule ya Msingi Mhunze, ambayo iko mbali na kijiji hicho. Kwa ujenzi wa shule hiyo Shikizi ya Ngando kwa kiasi kikubwa kutawapunguzia adha ya kutembea umbali mrefu wanayo ipata Wanafunzi hao wa kijiji cha Ngando:
Ujenzi huu shule shikizi ya Ngando unao jengwa kwenye eneo la ekari saba, kwa namna moja ama nyingine utapunguza Mlundikano wa wanafunzi katika shule ya Msingi Mhunze ambayo kwa sasa ina jumla ya Wanafunzi 2492.
KATA YA BUDALABUJIGA
Sehemu ya Mbele ya jengo la Maabara ya Shule ya Sekondari Budalabujiga likiwa katika hatua za Mwisho
|
Sehemu ya Nyuma ya Jengo la Maabara ya Shule ya Sekondari Budalabujiga iliyobp Wilayani Itilima |
Kamati ikiwa katika Kata ya Budalabujiga ilijiridhisha na maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Vyumba vitatu vya Maabara Katika shule ya Sekondari ya Budalabujiga.
Sanjari na kuridhika huko baadhi ya wajumbe walimtaka Mkurugrnzi wa Halmashauri ya Wilaya Itilima kupeleka pesa haraka za ukamilishaji wa mradi huo ambao Mwenge wa Uhuru utapita katika eneo hilo kuuzindua.
Akitoa maelezo ya utekelezaji wa Mradi huo, Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi, ambaye pia ni mkuu wa shule ya sekondari Budalabujiga Mwl. Zakaria Angelo alisema Mpaka sasa Mradi umeshatumia Milioni 25, na ili ukamilike Mradi unahitaji shilingi Milioni 30. Kwa mchanganuo ufuatao
Vitu vinavyo hitajika
Vigae: 8,500,000/-
Saruji mifuko 60 sawa na 1,080,000
Mfumo wa maji gesi 15,600,000/-
Stuli 75@ 40,000/ =3,000,000/-
Pcv =1,000,000/-
Dharura 2,000,000/-
Jiwe la Msingi Mradi huu wa ujenzi wa vyumba vitatu vya Maabara, liliwekwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim M.Majaliwa mnamo tarehe 04/03/2016
KATA YA NKOMA
Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Maji Mhe. Robert F. Jongela (katikati) akisikiliza maelezo ya ya Mkuu wa Idara ya Maji Eng: Goodluck Masige,Katika katika eneo la Mradi wa Maji, Nkoma.
|
Kamati ya Elimu, Afya na Maji ilipitia Mradi kipolo wa Maji Nkoma ambapo Mkataba wa Mkandarasi wa awali ulitenguliwa na taratibu za kumpata mkandarasi mpya zimekamilika na anatarajiwa kuanza kazi karibuni, kwa mujibu wa Eng: Goodluck Masige.
Hata hivyo ushauri wa Kamati ulimtaka Eng. Masige kwa niaba ya Mkurugenzi ahakikishe kazi inaanza mara moja.
Kamati ya Afya, Elimu na Maji ilihitimisha ziara yake kwa siku hiyo katika kata ya Nkoma katika Shule ya Sekondari ya Nkoma, ambapo kuna ujenzi wa Mabeni mawili ya wanafunzi wa kike, ambap Bweni moja limefadhiliwa na Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China, na lapilli ni kwa Nguvu za Wananchi.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nkoma wakishiriki katika umwagiliaji wa Jengo la Bweni la Watoto wa kike katika shule hiyo.
|
Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na maji Mhe,Robert F. Jongela akitoa maelekezo ya Kamati, kwa kamati ya Ujenzi wa Mabweni katika Shule ya Sekondari Nkoma. |
Maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo ambao unatarajiwa kuzinduliwa rasmi na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli sambamba na Balozi wa China nchini Tanzania upo katika hatua za ukamilishwaji na mafundi wanafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha, kufikia tarehe 15/08/2018 jengo liwe limekabidhiwa kwa mamlaka husika kwa matuzi.
Katika Majumuisho Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Maji Mhe. Robert F. Jongela alitoa siku 14 za ukamilishwaji wa mradi huo na kuahidi atafanya ziara ya kustukiza usiku, kujiridhisha kama mafundi ahadi yao yakufanya kazi usiku wanaitekeleza.
Akitoa taarifa fupi ya Mapato na Matumizi Mwenyekiti wa kamati ya Ujenzi ambaye ni Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Sarah Matonya kwa Kamati hiyo, alisema “Ujenzi unaendelea Vizuri na mpaka sasa tumesha pokea takribani shilingi million 89.2 kwa ajiri ya ujenzi wa Bweni la wanafunzi wa kike lenye idadi ya vyumba 20 vya kulala . fedha hiyo tulipokea tarehe 08/303/2018 na mpaka sasa tumetumia shilingi milioni 78.6/- zimebaki shilingi milioni 10.6.”
Ufadhili wa ujenzi wa Bweni haya ya Nkoma ulitolewa na Ubarozi wa Jamhuri ya Watu wa China kwa kuahidi kutoa shilingi milioni 178.4, katika kuunga mkono Juhudi za Halmashauri ya Wilaya ya Itilima kwa kushirikiana na Wananchi wa Kata ya Nkoma waliona ni vyema kuongeza nguvu ili kupata bweni la pili lenye idadi ya vyumba sawa na Bweni la awali, hivyo wananchi hao walishiriki juhudi hio kwa kuleta Mchanga, mawe Kokoto na nguvu kazi, pamoja na kushiriki zoezi zima la ujenzi kama kushiriki kuchimba msingi,, kujaza kifusi ndani ya Bweni, kumwaga jamvi pamoja na kushiriki shughuli zingine za ujenzi.
KAMATI YA UCHUMI, UJENZI NA MAZINGIRA
Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mzingira chini Uwenyekiti wa Diwani wa Chinamili Mhe. Nindwa S. Bukanu ulianza ziara yake katika kata ya Nkoma, kamati hii ilijikita katika Kuangalia Mchakato Mzima wa Manunuzi ya Pamba na Usafirishaji wake katika baadhia ya Vyama vya Msingi (AMCOS) na kubaini kasoro kadhaa na kutoa ushauri.
Wajumbe wa Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira wa Halmashauri ya Itilima wakiwa katika chama cha Msingi cha Nilamagembe Nkoma Kukagua kukagua shughuri za manunuzi na Masafirisho ya Pamba kituoni hapo.
|
Kamati ilitembelea AMCOS zifuatazo Nimalamagembe ya Nkoma, Lugunamo ya Kijii cha Namgagani, Mwanco ya Mwamapalala, Hapana Wanyonyaji ya Ngeme katika Vyama hvi vya Msingi changamoto zifuatazo zilijitokeza
Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira ilikamirisha ziara yake kwa Kuangalia maendeleo ujenzi wa Jengo lenye madarasa Matatu, la shule shikizi ya Msingi Mlimani, iliyopo katika Kijiji cha Mlimani, kata ya Zagayu.
Shule hiyo inayo jengwa kwa Nguvu za Wananchi, Ufadhili wa Mbunge wa Jimbo la Itilima Mhe. Njalu Silanga na mapato ya ndani ya kijiji hicho ambayo yanategemea malipo ya pango la Minara ya mawasiliano kutoka kampuni ya Voda na Airtel.
Akitoa Ushauri kwa Diwani wa Kata ya Zagayu Mhe Kuzenza A Kuzenza, Diwani wa Kata ya Bumera Mhe. Mboje N. Mulli alisema itabidi Mlimani Make na Serikali ya Kijiji Muinue Maboma matatu ili mpata pesa za Equip.
Kuhusu hali ya Wananchi kujitolea Mwenyekiti wa Kikiji hicho cha mlimani Ndg. Jiji Madoka alisema “wananchi wanashauku kubwa ya kuona watoto wao wanatembea umbali mfupi wa kenda kupata elimu na ndiyo maana wakawa wepesi kuitikia wito wa ujenzi wa shule hii shikizi”
Shule hiyo inaeneo la ekari tisa na robo tatu na mwenye eneo keshalipwa.
Ziara hizi za Waheshimiwa Madiwani zilikamilishwa na KAMATI YA FEDHA, UTAWALA NA MIPANGO
Kamati ilianza ziara yake katika Kijiji cha Nanga, kilichopo katika Kata ya Chinamili, kwa kutembelea Chama cha Msingi Nanga, Kamati ilihoji manunuzi na masafirisho ya pamba katika Amcos hiyo, ambapo katibu wa Amcos hiyo Ndg Dadu Yombi alijibu kuwa mpaka tarehe 18/07/2018 manunuzi yalikuwa ni tani 185 na masafirisho yalikuwa ni tani 163.
KATA YA IKINDILO
Jengo la Wodi ya Wazazi la Kituo cha afya Ikindilo likiwa katika Hatua za Mwisho za Ukamilishhwaji. |
Jengo la Chumba cha Upasuaji la Kituo cha Afya Ikindilo, likiwa limeunganishwa na Njia za kutembelea, zinazo elekea katika Wodi ya wazazi |
Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango wakisikiliza maelezo ya Mkuu wa Idara ya Ujenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Eng. Furaha Mwampulo wakiwa katika jengo la Kufuria la Kituo cha Afya Ikindilo |
wajumbe wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango, wakikagua ujenzi wa jengo la kuhifadhia Maiti, katika kituo cha Afya Ikindilo |
Baadaye kamati ya Fedha, Utawala na Mipango chini ya Uwenyekiti wa Salum L. Mrushu ulifika Katika Kituo cha Afya Ikindilo kuangalia Maendeleo ya Ujenzi wa Wodi ya Wazazi, Chumba cha upasuaji, Chumba cha kuhifadhia Maiti, Maabara pamoja na chumba cha kufulia.
Akitoa maelezo ya Mradi huo, Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Ikindilo Dkt. Japhet Bahini alisema “ujenzi wa kituo hiki, ulianza tarehe za mwanzoni za Mwezi Desemba mwaka 2017, changamoto zilizo jitokeza, na kufanya Mradi uchelewe ni Mvua za masika, zilikwamisha usafilishaji wa vifaa vya ujenzi na kwa upande wa Wananchi, walishindwa kufuata mawe milimani, kwani mazingira kwa kipindi hiko haya kuwa rafiki”
Akiongeza kwenye maelezo ya Mganga Mfawidhi, Kaimu Mkuu wa Idara ya Ujenzi Eng. Furaha Mwampulo alisema “ kuchelewa kumalizika kwa Mradi kulisababishwa na vitu vingi ikiwemo kuchelewa kufika kwa mabati kutoka Alaps Mwanza”
Hata hivyo Kaimu Mkuu wa Idara ya Mipango na Takwimu (W) Ndg. Kita Charles alimtaka Mganga Mfawidhi, Dkt. Bahini achangamke na awe anayafanyia kazi, maelekezo anayopewa na kikosi kazi kwa wakati, ili kwenda na ratiba.
Akihitimisha ziara hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango Mhe. Mrushu alisema “jitihada ziongezwe katika usimamizi na tukumbuke tuna ugeni Mkubwa, taarifa za Mradi ziwekwe vizuri, na suala la muda lizingatiwe.
Ujenzi katika kituo hicho cha Afya, hususani ujenzi wa Wodi ya Wazazi, Chumba Cha Upasuaji, Maabara, Chumba cha kuhufadhia Maiti, Chumba cha Kufulia na Njia za kupitia Wangonjwa, umefadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kutoa shilingi Milioni 250/- na Shilika la Umoja wa Mataifa linalo shughulikia Idadi ya watu (UNFPA) ambalo limetoa shilingi milini 275/- kwa kufadhili ujenzi huo.
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa